loader
Asilimia 18 ya Watanzania wana selimundu

Asilimia 18 ya Watanzania wana selimundu

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Tiba Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Hedwiga Swai wakati wa maadhimisho ya Siku ya Selimundu Duniani.

Maadhimisho hayo kitaifa yanafanyika leo mjini Dodoma. Alisema hospitali hiyo imejipanga kutoa elimu na huduma ya damu kwa wagonjwa hao.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Selimundu Tanzania, Grace Rubambey alisema bado Tanzania haijafanya jitihada madhubuti za kupambana na ugonjwa huo hivyo kuongeza idadi ya wagonjwa wa selimundu.

Alisema chembe nyekundu za damu za mtu wa selimundu zinafanana na mwezi mchanga na kwamba damu inashindwa kupita kwa urahisi na kuleta maumivu makali.

Mkuu wa Kitengo cha Afya katika Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Sarah Maongezi aliwataka wananchi kuacha imani potofu zinazopotosha kuhusu maisha ya wagonjwa wa selimundu.

"Mtu mwenye selimundu anaweza kuishi maisha marefu kama watu wa kawaida isipokuwa huwa wanasumbuliwa na tatizo la kuugua mara kwa mara,"alisema Maongezi na kuongeza kuwa,WAMA watahakikisha wanawasaidia wenye ugonjwa huo kupata matibabu sahihi na kutoa elimu ya kupima afya ili kutambua ugonjwa huo mara kwa mara.

AS Tanzania celebrates its 60th anniversary of independence on ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi