loader
ATCL yajipanga kununua ndege sita

ATCL yajipanga kununua ndege sita

Katika swali lake, Owenya, alitaka kufahamu ATCL inamiliki ndege ngapi na kati ya hizo, ni ngapi zimekodishwa na zinafanya safari kwenda wapi.

Baada ya kujibiwa kwamba ndege inayomilikiwa na ATCL ni moja, Owenya alisema ni aibu kwa shirika kuwa na ndege moja wakati liliwahi kumiliki ndege saba.

Ili kuondoa aibu hiyo, Mbunge huyo alipendekeza mali za shirika hilo, zikiwemo nyumba zake katika nchi mbalimbali, ikiwemo ya London, Uingereza, ziwekwe rehani ili kupata mkopo wa kununua ndege hizo.

Pia alipendekeza njia za ATCL kwenda katika nchi mbalimbali, hususani ya Dubai, katika nchi za Falme za Kiarabu, Uingereza na Marekani, zikodishwe kuongezea shirika hilo fedha za kujiendesha kwa kuwa kwa sasa halina uwezo wa kutumia njia hizo.

Akifafanua mipango ya Serikali ya kufufua shirika hilo, Dk Tizeba alisema mbali na kumiliki ndege hiyo moja aina ya Dash 8 Q 300 yenye uwezo wa kubeba abiria 50, ATCL pia imekodi ndege moja aina ya CRJ 200, yenye uwezo wa kubeba watu 50 kutoka Kampuni ya AXMAX ya Kenya.

Kwa mujibu wa Dk Tizeba, ndege inayomilikiwa na ATCL, inatoa huduma zake katika njia za Dar es Salaam, Kigoma, Mtwara na Bujumbura, nchini Burundi.

Aidha ndege iliyokodishwa, inatoa huduma zake katika njia za Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Mtwara na Hahaya nchini Comoro.

Hali ya sasa ya ATCL, ni tofauti na ilivyokuwa miaka michache iliyopita ambapo haikuwa na ndege hata moja iliyokuwa ikitoa huduma.

Mwaka 2011, aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu, akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR Mageuzi) bungeni, alisema ATCL ilianzishwa kwa kupewa ndege 11 mwaka 1973, lakini mpaka mwaka huo 2011, hakukuwa na ndege hata moja iliyokuwa ikifanya kazi.

Akifafanua mipango ya Serikali ya hivi karibuni, Dk Tizeba alisema ATCL ina mpango wa kununua ndege mbili, kwa mfumo wa kibiashara wa kukodi huku malipo ya ununuzi yakifanyika taratibu. Ndege hizo aina ya D8 Q 400, zenye uwezo wa kubeba abiria 78 kila moja baada ya kununuliwa, zitaongeza wigo wa huduma za ATCL katika njia za Nairobi nchini Kenya, Kigali nchini Rwanda na nchini Uganda.

Kwa mujibu wa Dk Tizeba, ununuzi wa ndege hizo utafanyika baada ya kukamilika kwa taratibu za kisheria na kibiashara ambazo zinafuatwa hivi sasa, ili ndege hizo zianze kufanya kazi mwishoni mwa mwaka huu.

Baada ya kukamilika kwa utekelezaji wa mpango huo, ambao utafanya ATCL kurusha ndege nne na kutoa huduma za ndani na katika nchi za Afrika Mashariki, Dk Tizeba alisema utafuata utekelezaji wa ununuzi wa ndege nyingine mbili.

“Kuna mpango wa kununua ndege mbili ndogo aina ya Y12E, kwa mkopo nafuu wa Exim Bank kutoka China kwa Serikali ya Tanzania, kila moja ina uwezo wa kubeba abiria 20”, alisema.

Mbali na ndege hizo, pia Serikali kwa mujibu wa Dk Tizeba itanunua ndege mbili aina ya ERJ 170 na ERJ 190, zenye uwezo wa kubeba abiria 80 mpaka 100 kutoka nchini Brazil.

“Ndege hizi zitanunuliwa kwa utaratibu wa mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Brazil,” alisema Dk Tizeba na kusisitiza kuwa baada ya kupatikana kwa ndege hizo, ATCL itaanza kutumia njia zake za kimataifa kwa kuwa bado zipo.

WAKALA wa Usafi ri wa Mabasi ...

foto
Mwandishi: Joseph Lugendo, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi