loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Azam, KMKM zaanza kwa sare Kagame

Azam FC ikicheza michuano hiyo baada ya waandaaji, Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuwafukuza Yanga kwa kupeleka timu ya vijana, ilishindwa kuitambia Rayon Sports ya Rwanda kwenye Uwanja wa Amahoro mjini Kigali.

Awali, KMKM ilifungua dimba na Atlabara ya Sudan Kusini na kwenda sare ya bao 1-1 kwenye uwanja huo wa Amahoro katika mechi hiyo ya Kundi A ambalo pia lina Azam FC, Rayon na Adama ya Ethiopia.

KMKM ilipata bao la kuongoza katika dakika ya 30, baada ya mchezaji wa Atlabara, Karim Mutawakili kujifunga kwa kichwa. Kama ilivyokuwa kwa Atlabara KMKM nao walijifunga bao dakika ya 45 baada ya Makame Mngwali kujaribu kuuokoa mpira wa krosi.

Katika mechi ya Azam FC na Rayon Sport, vijana hao wa Chamazi itabidi wajilaumu wenyewe kwa kutopata ushindi baada ya kupoteza nafasi nyingi nzuri kupitia kwa Kipre Tchetche, Himid Mao na John Bocco.

Tchetche, ambaye ni mchezaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, ndiye aliyepoteza nafasi nyingi zikiwamo katika dakika za 43, 58 na 63 ambayo ilikuwa nzuri zaidi, lakini akiwa anamtazama kipa wa Rayon, alipiga shuti la ovyo la mguu wa kushoto na kutoka nje.

Katika mchezo mwingine wa pili ambao ulikuwa wa Kundi B, KCCA ya Uganda ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya. Bao la Gor Mahia lilifungwa dakika ya 27 na Dan Sserunkuma.

Mabao ya KCCA yalifungwa na Brian Majwega dakika ya 52 na Brian Umony dakika ya 88. Leo itakuwa Vital’O ya Burundi dhidi ya Benadir ya Somalia, Polisi Rwanda dhidi ya El Merreikh ya Sudan na APR ya Rwanda dhidi ya Atletico ya Burundi.

MWISHO wa ngebe ni leo baada ya dakika ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi