loader
Bei ya ufuta Lindi yayumba

Bei ya ufuta Lindi yayumba

Mkuu wa mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe wa kikao cha ushauri ngazi ya mkoa (RCC). Alisema msimu uliopita bei zilikuwa juu na ilifikia mpaka Sh 3,500 kwa kilo moja.

“Sisi viongozi tuwasimamie wakulima kwa kuhakikisha bei iliyopangwa ya Sh 2,500 ndiyo inatakiwa wanunuzi wanunue siyo chini ya hapo, itakuwa hatuwatendei haki wakulima wetu,” alisema Mwananzila.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Peter Malekela alilalamikia kitendo cha baadhi ya wafanyabiashara kushusha bei na kukwepa kulipa ushuru wa zao hilo.

Kwenye kikao cha baraza la madiwani lililofanyika hivi karibuni alisema kuwa licha ya kushusha bei inaenda sambamba na kukwepa kulipa ushuru wa mamlaka hiyo.

Naye Diwani wa kata ya Kiranjeranje, Ali Mtotela alisema kuwa hata viongozi wenyewe wanahusika na ukwepaji wa kulipa ushuru wa halmashauri hiyo.

foto
Mwandishi: Kennedy Kisula, Lindi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi