loader
Benki M yapata faida bilioni 5.05/-

Benki M yapata faida bilioni 5.05/-

Ofisa Mtendaji Mkuu, Jacqueline Woiso alisema jijini Dar es Salaam faida kabla ya kodi iliyopatikana ni Sh bilioni 5.05, ukilinganisha na faida ya Sh bilioni 4.63 mwaka jana.

“ Mafanikio katika kupata faida yanatokana na utendaji unaozidishwa na uimara katika kufanya miamala ya kibenki na usafirishaji wa fedha za kigeni,” alisema.

Alisema hisa iliongezeka kutoa Sh bilioni 68.11 kutoka kwenye Sh bilioni 64.63 kipindi kilichopita, wakati mizania ikifikia bilioni 555.

Wakati benki inaanza 2007, mizania ilikuwa Sh bilioni 37. Woiso alisema kamisheni imefikia Sh bilioni 4.5 kutoka kwenye Sh bilioni 3.8, ikiwa imekua kwa asilimia 10 wakati mikopo ikiongezeka hadi kufikia Sh bilioni 456.

Wakati huo huo, Woiso alisema Benki M Tanzania iko katika mchakato wa mwakani kuingia katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

“ Kwa mwaka huu wanahisa hawajafikia uamuzi wa kuingia kwenye soko la hisa, kwa mwakani huweda wakafikia uamuzi huo,” alisema.

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi