loader
Dstv Habarileo  Mobile
Benki ya Dunia yapiga jeki elimu kupitia BRN

Benki ya Dunia yapiga jeki elimu kupitia BRN

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Philippe Dongier, alisema pamoja na msaada huo, benki hiyo pia imeidhinisha msaada wa kuimarisha Sekta ya Elimu ya Sayansi na Teknolojia kwenye elimu ya juu, lengo likiwa ni kuzalisha wataalamu wengi zaidi ambao wataweza kuendana na mahitaji ya uchumi wa sasa.

Akizungumzia msaada huo wa kuimarisha sekta ya elimu kupitia BRN, Dongier alisema takribani muongo mmoja sasa, zaidi ya watoto milioni moja wenye umri wa kuanza shule nchini waliandikishwa na kwamba jambo muhimu hivi sasa ni kuimarisha ubora wa elimu inayotolewa.

Alisema Benki ya Dunia imeanzisha programu mpya ambayo inaangalia matokeo ya sekta mbalimbali na kwa mara ya kwanza inasaidia sekta ya elimu nchini ambapo fedha hizo zinatumika kwa miaka minne kuanzia sasa.

Kwa upande wake, Mtaalamu wa Masuala ya Elimu wa Benki hiyo, Arun Joshi alisema kupitia programu hiyo mpya ya elimu kutoka Benki ya Dunia, Tanzania ambayo ni mshirika wake itafaidika kwa kuhakikisha watoto wa shule za msingi na sekondari wanasoma kwenye mazingira bora.

Katika mpango wa pili wa kuimarisha elimu ya sayansi na Teknolojia, alisema dola za Marekani milioni 15 zitatolewa ili kuimarisha eneo hilo.

Alisema kila mwaka watu 800,000 huingia kwenye soko la ajira na wengi wao wakiwa na upungufu wa ujuzi hivyo kufanya wakose ajira na kwamba mpango huo umelenga kuimarisha uwezo wa nguvukazi hiyo ili waweze kuingia sokoni na kushinda kwa kuwa watakuwa na uwezo na ujuzi.

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi