loader
CAG ataka weledi wakaguzi wanaokwenda UN

CAG ataka weledi wakaguzi wanaokwenda UN

Alitoa rai hiyo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wakaguzi wanaokwenda kufanya kazi katika vikosi vya ulinzi wa amani chini ya UN. Wakaguzi hao wako chini ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (NAOT).

Alisema mwaka juzi, Naot iliteuliwa kuwakilisha Afrika kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakaguzi wa Hesabu za UN.

Moja ya majukumu yake ni kufanya kazi za ukaguzi katika mashirika ya UN hususani katika vikosi vya ulinzi wa amani.

"Tanzania imefanikiwa kufanya vyema katika mzunguko wa kwanza uliokamilika Julai mwaka jana na hiyo ni baada ya wakaguzi waliohusika, kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa,” alisema.

Alisema katika kipindi hicho cha mzunguko wa kwanza, Tanzania ilikuwa ikifanya kazi hiyo ikiwa chini ya usimamizi wa Ofisi ya Mkaguzi kutoka China.

Juni mwaka huu inakamilisha kazi yake na kuiacha Tanzania ikiendelea na kazi. Mafunzo hayo yanayotarajiwa kumalizika Machi 28 yanatolewa na mtaalamu kutoka Ofisi ya Mkaguzi ya China (CNAO), Chen Wechun.

Anashirikiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa anayeiwakilisha Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania (UN-NAOT) Salhina Nkumba.

MWENGE wa Uhuru unaendelea ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi