loader
Chiza: Saccos zisiwe vichaka vya wahalifu

Chiza: Saccos zisiwe vichaka vya wahalifu

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na chama cha kuweka na kukopa (Saccos), alipokuwa akikagua mabanda kwenye Maonesho ya Wakulima (Nanenane) mjini hapa.

Alisema umoja huo, unatakiwa uwe thabiti, siyo kulalamika, kwani viongozi ambao sio waadilifu, ndio waliochaguliwa na wao wenyewe kwa hiyo wana uwezo wa kutosha, kuwaondoa wakati wakibainika kuwa hawana uzalendo.

“Vyama vyetu vya ushirika, kukopa na kuweka tusivifanye sehemu ya kuwa vichaka, ni muhimu kuwa makini sana ili tupate maendeleo ya kiuchumi,” alisema Chiza.

Alisema baadhi ya watu walikuwa wanadai sherehe za Nanenane zinazofanyika kitaifa Lindi, hazingekuwa nzuri, kutokana na mazingira yake. Lakini, alisema sherehe hizo zilifana na serikali ilitumia Sh milioni 600 kufanikisha sherehe hizo kitaifa katika mkoa wa Lindi.

MGODI wa kati wa madini ya dhahabu ...

foto
Mwandishi: Kennedy Kisula, Lindi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi