loader
Dstv Habarileo  Mobile
Diamond, Jaydee washinda tuzo Marekani

Diamond, Jaydee washinda tuzo Marekani

Tuzo hizo zijulikanazo kama African Muzik Magazine Awards zilitolewa Julai 26, mwaka huu kwenye eneo la Eisemann Center Richardson, Texas, Marekani.

Diamond ameshinda katika kipengele cha Mwanamuziki Bora wa Kiume kwa Afrika Mashariki, wakati mwimbaji nyota, Jaydee ameshinda katika kipengele cha Mwanamuziki Bora wa Kike Afrika Mashariki.

Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Diamond ameandika ujumbe akimshukuru Mungu kwa baraka zake pamoja na mashabiki wake, wasanii wenzake pamoja na waandishi wa habari.

Mwimbaji huyo nyota wa kizazi kipya kwa sasa, alisema amekuwa akijihusisha kwenye tuzo nyingi ambazo amefikia kwenye hatua ya ushindani na kwa hii amefikia hatua ya kushinda tuzo hiyo.

Aliendelea kuandika kuwa amekuwa akifanya kazi nzuri ambayo imekuwa ikikubalika ndani na nje ya nchi na kuahidi kuendelea kufanya vema zaidi.

Kwa upande wake, aliandika akiwashukuru mashabiki wake kwa kumwezesha kuchukua tuzo hiyo. Alisema amekuwa akifanya kazi kwa bidii na kwa muda mrefu na kisha kusisitiza kuwa ushindi huo ni matunda ya kufanya kazi vema.

Pia kwenye hafla hiyo wasanii kutoka nchi mbalimbali walitunukiwa tuzo ambapo DJ Bora Afrika 2014, aliyeshinda ni Dj Black (Ghana), wakati DJ Bora Mwafrika katika Marekani ni Dj Josh wa (Kenya), Video Bora ya Mwaka Flavour (Nigeria) na Msanii Bora wa Kiume Afrika Magharibi, Davido (Nigeria).

Tuzo ya wimbo wa mwaka ilikwenda kwa Kcee (Nigeria) huku Davido wa Nigeria akiibuka tena kama msanii wa mwaka 2014 huku Tuzo ya Leadership in Music Award 2014 ilienda kwa 2face Idibia.

Tuzo ya mwanamuziki mkongwe wa mwaka ilienda kwa Yvonne Chaka Chaka wa Afrika Kusini huku tuzo ya kutambua uendelezaji wa muziki ilikwenda kwa Chifu Dk Godswill Akpabio.

YANGA leo saa 1:00 usiku itashuka dimbani kuikabili ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi