loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DIMBWI LA MAHABA: Epuka uhusiano usio na upendo

Upendo ndio msingi mkuu wa uhusiano wowote, kwani ili watu wawili wakubaliane kuwa kitu kimoja, lazima kuwe na vitu vinavyowafanya kila mmoja avutiwe na mwenzake.

Na endapo, hali hiyo ya upendo ikiegemea upande mmoja na mwingine kubakia tu kwa ajili ya mazoea ni wazi kuwa uhusiano huo hauwezi kudumu na kama utaendelea, basi utatawaliwa na matendo yenye kuvunja moyo, maumivu na hatimaye kuvunjika.

Na ukweni ni kwamba ili mapenzi yaweze kuwa bora kwa kila aliye katika uhusiano, huwa ni vyema kila mmoja kuiona thamani ya mwenzake. Hivyo, basi mtu anapokuwa katika uhusiano wowote ni vyema kuchukua tahadhari na kumchunguza vyema mwenza wake, kuhusu upendo alionao dhidi yake.

Na hilo linaonekana dhahiri kupitia namna mwenza wako anavyokuthamini kwani unapokuwa na uhakika kama anakupenda na kukuthamini hapo ndipo nafsi yako itatulia na kuwa na amani.

Endapo upo kwenye uhusiano na mtu ambaye huna uhakika na hisia zake au ki ukweli huna mapenzi naye ni hatari si kwakwe tu bali hata kwa afya yako kwani kamwe huwezi kuufurahia uhusiano husika.

Na madhara yake ni kwamba, hutoweza kumtimizia mambo ya msingi kama vile upendo, uaminifu na hata heshima kwani thamani yake kwako haitokuwa kubwa kwa kuwa huna upendo wa dhati kwake.

Kifupi huo utakuwa ni uhusiano wa kitumwa. Mbaya zaidi katika dunia hii iliyojaa watu wa kila aina, wapo watu wengi ambao ni matapeli katika uhusiano, watu wa aina hiyo huwa kwenye uhusiano tena wa muda mrefu tu kwa malengo yao ya kibinafsi.

Watu hao tena wanawake kwa wanaume, huwa kwenye uhusiano husika huku tayari wakiwa na wenza wao ambao wanawapenda kwa dhati lakini hutumia uhusiano huo wa kughushi pale wanapobughudhiwa na wenza wao wanaowapenda au kujifurahisha tu.

Mara nyingi uhusiano wa aina hiyo, hukuta mwenza mwingine akimpenda mwenzake kumbe mwenzake ni tapeli na ndio maana wengi hulia na kudai kuwa mapenzi ni magumu. Jambo la msingi, ukiwa katika uhusiano usijibweteke na kuridhika kwa kila kitu, jihangaishe na kujiridha kama kweli uhusiano ulio nao ni wa upendo wa dhati au kudanganyana kabla haujachelewa.

Kumbuka kila binadamu ana haki na hadhi ya kuthaminiwa, kupendwa na kuheshimiwa bila kujali mwonekano au uwezo wa kipato chake. Wahenga walisema aheri ya nusu shari kuliko shari kamili.

Naamka asubuhi,  sioni kilongalonga, 
Napapasa kitandani,  hamadi hiki hapa,  

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi