loader
Dstv Habarileo  Mobile
Diouf, Amigolas kupamba vipaji Miss Mashariki

Diouf, Amigolas kupamba vipaji Miss Mashariki

Akizungumza jana Dar es Salaam, Mratibu wa shindano hilo, Alex Nikitas alisema pia litafanyika kwenye Ukumbi wa Maisha Plus, Kibaha, Mkoa wa Pwani na kuhudhuriwa na Mbunge wa Kibaha Mjini, Silvestry Koka.

Nikitas alisema maandalizi ya shindano hilo yamekamilika na onesho litaanza saa 2.00 usiku huku warembo wakichuana katika vipaji mbalimbali kama kuimba, kucheza muziki wa kisasa, wa asili na ya nje ya nchi.

“Warembo wapo katika maandalizi makali tayari kuchuana katika mashindano hayo, mbali ya vipaji, pia warembo hao watatoa misaada mbalimbali kwa vituo vya watoto yatima katika mkoa huo,” alisema.

Alisema awali walipanga kufanya shindano hilo siku ya Idd Pili, lakini kutokana na muda wameamua kulifanya leo ili kuwapa muda zaidi warembo kwa ajili ya mazoezi ya kuwania taji la mrembo wa Kanda ya Mashariki Agosti 8, kwenye Hoteli ya Nashera mkoani Morogoro.

Alisema warembo hao wataondoka Mkoa wa Pwani keshokutwa tayari kwa kambi ya mwisho kwenye Hoteli ya Usambara Safari Lodge chini ya Miss Kanda ya Mashariki wa mwaka jana, Diana Laizer.

YANGA leo saa 1:00 usiku itashuka dimbani kuikabili ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi