loader
Dk Bilal afunda wafanyabiashara ndogo kemikali

Dk Bilal afunda wafanyabiashara ndogo kemikali

Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal alisema hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam na kusema taasisi ya saratani ya Ocean Road, imekuwa ikipokea wagonjwa wapya 5,000 wa saratani.

Alisema tabia na vitendo hivyo vya kuchanganya vyakula na kemikali, si vya kiungwana. Ameahidi kwamba serikali itaendelea kusimamia na kuhakikisha matumizi sahihi ya kemikali yanakuwepo.

Alisema kemikali zisipotumiwa vizuri, zina madhara makubwa kwa binadamu ikiwemo kusababisha ongezeko la ugonjwa wa saratani na maradhi mengine.

Alisema kemikali hutumika kuzalisha mbolea, dawa za kuulia wadudu, kutengeneza dawa za hospitalini, ujenzi wa nyumba kama saruji, rangi, mbao na mabati na matumizi mengine mengi.

Aidha alisema changamoto kubwa katika hilo ni namna bora na salama ya kutumia kemikali hizo zisilete madhara kwa afya ya watu na kuziepusha kuingia kwenye mfumo wa ikolojia na kuchafua mazingira.

Hata hivyo alisema madhara ya kemikali yanaweza kuwa ya muda mrefu au mfupi kulingana na kiwango kitakachoingia mwilini. Kemikali zinaweza kuharibu mifumo ya fahamu, damu, uzazi na hata mifupa.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments