loader
Exim wapata faida bilioni 9.6/-

Exim wapata faida bilioni 9.6/-

Kaimu Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim jijini Dar es Salaam, Issa Hamisi alisema jana ukuaji huo wa mapato unaashiria mafanikio yatokanayo na vyanzo vya mapato vya benki.

“Benki yetu ipo katika mwelekeo mzuri. Tupo katika hatua nzuri ya kufikia malengo yetu. Matokeo yetu ya robo ya pili yanaonesha tumeendelea kufanya vizuri mwaka huu,” alisema.

Alisema faida ghafi ya riba, imekuwa kwa asilimia 36 katika kipindi sawa na hicho mwaka jana mpaka Sh bilioni 14.3.

“Biashara ya fedha za kigeni imekua katika robo hii na asilimia 33 imeongezeka kwenye robo ya pili ikilinganishwa na mwaka jana.”

Alisema gawiwo lililopokewa katika robo ya pili kutoka katika vyanzo vya uwekezaji kwa Benki ya NMB na tawi la Comoro kwa mwaka jana limeonesha kuwa chanya katika matokeo yao mazuri.

Pato la tozo na kamisheni limeongezeka kwa asilimia 19 kutoka katika robo ya mwaka uliopita hadi Sh bilioni 6.2. lililotokana na kukua kwa biashara ya fedha za kigeni na bidhaa za kifedha za biashara baada ya utekelezaji wa mpango mkakati wa miaka mitatu.

Kwa mujibu wake, pato kutoka katika vyanzo vya uwekezaji limekua kwa asilimia 184 ikilinganishwa na kipindi hicho mwaka jana, hadi Sh bilioni nne, litokanalo na ongezeko la pato la gawiwo lililopokelewa.

Alisema katika jitihada za kuimarisha nafasi yake ya kiushindani benki imejikita katika muundo wa kibunifu wa biashara ndogo ambao umeboresha mawasiliano na wateja na uendeshaji wa karibu zaidi wa matawi yote.

Muundo huo mpya wa Menejimenti katika matawi umeanzishwa mwaka huu.

MGODI wa kati wa madini ya dhahabu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi