loader
Fastjet kwenda Harare

Fastjet kwenda Harare

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo leo, Mwenyekiti Mtendaji na Ofisa Mtendaji wa muda wa Fastjet, Ed Winter alisema kwamba safari hiyo itaanza Agosti, mwaka huu.

Winter alisema Fastjet itafanya safari mara mbili kwa wiki kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Harare ambapo nauli ya chini zaidi itakuwa ni Dola za Marekani 50 (Sh 84,059).

“Tunachukua nafasi hii kutangaza safari ya tatu ya kimataifa ya Fastjet kutoka Tanzania, kwa sababu tayari inakwenda Zambia na Afrika Kusini,” alisema Winter.

Naye Waziri wa Usafirishaji wa Zimbabwe, Dk Obert Mpofu, akizungumza wakati wa uzinduzi wa safari hiyo alisema anaishukuru Kampuni ya Fastjet kwa kuanzisha safari hiyo kwa gharama nafuu na itakuwa na msaada mkubwa kwa wananchi wa Zimbabwe.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi