loader
Dstv Habarileo  Mobile
Fedha, faida BoT inajadilika

Fedha, faida BoT inajadilika

Alisema hayo jana alipokuwa akichangia katika Bunge Maalumu la Katiba mjini hapa. Kuhusu uanzishwaji wa akaunti ya pamoja ya fedha za Muungano ambayo mchakato wake umeshaanza Zanzibar, alisema ni fursa ya pekee kupitia Katiba mpya, kuingizwa humo humo.

Ghasia aligusia pia kuhusu makato ya kodi mara mbili mbili kwa wafanyabiashara na kueleza kuwa kuanzisha serikali tatu, kodi hiyo itaongezeka maradufu badala ya kupungua na kwamba, serikali tatu ni kuongeza madaraka.

“Tufikirie baada ya miaka kadhaa tutakuwa na mawaziri wakuu, makamu wa rais wangapi, wenzetu wanataka serikali tatu labda nao Ukawa (kundi la wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi) wataokota kimojawapo.

Alishauri Bunge Maalumu litakalokutana Agosti, muda wa kujadili sura za rasimu katika Kamati uongezwe na masuala yakishajadiliwa kwenye kamati, kuwe na muda mfupi wa kuwasilisha katika kikao cha Bunge zima, ili kupunguza kuchezea muda na wajumbe kuishia kutukanana na kuwakashifu waasisi wa Taifa.

Ghasia aliwafananisha wajumbe wanaotukana kama wanaume ambao hawajaenda jandoni na kama walienda hawakufundwa wakafundika hivyo kwa utaratibu wa jando, watu wa aina hiyo wanatakiwa kurejeshwa kufundwa upya.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imepata nmkopo ...

foto
Mwandishi: Waandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi