loader
Fedha yasakwa kukarabati Mombo-Lushoto

Fedha yasakwa kukarabati Mombo-Lushoto

Hayo yalisemwa na Rais Jakaya Kikwete jana wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la ukarabati wa barabara ya Korogwe- Mkumbara yenye urefu wa kilometa 76, mradi unaotekelezwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia.

“Wakati tunapoelekea kutangaza zabuni huku Serikali nayo ikiwa mbioni kutafuta fedha zitakazotosheleza kazi ya matengenezo hayo ili barabara ya Mombo- Lushoto irudi katika kiwango chake cha kawaida hasa ikizingatiwa kwamba ni chakavu sana kutokana na kujengwa zamani”, alisema.

Akizungumzia mchakato wa ujenzi wa barabara ya Tanga -Pangani –Saadani hadi Bagamoyo kwa kiwango cha lami, alisema uko katika hatua nzuri na kwamba lengo ni kuwezesha wasafirishaji wanaotoka Mombasa hadi Dar es Salaam kutolazimika kufika hadi njiapanda ya Segera.

Awali akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kumkaribisha Rais kuhutubia wananchi Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alisema Serikali imetenga zaidi ya Sh bilioni 10.9 kutoka kwenye mfuko wa barabara kwa ajili ya kufanyia matengenezo barabara kuu na za mkoa.

Naye Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Kanda Afrika Mashariki, Philpe Dongier alisema benki hiyo imetoa mikopo ya dola biloni 334.5 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara nchini .

MWENGE wa Uhuru unaendelea ...

foto
Mwandishi: Anna Makange na Nakajumo James, Korogwe

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi