loader
Harufu ya ufisadi yanukia barabara ya mita 876

Harufu ya ufisadi yanukia barabara ya mita 876

Uamuzi huo umechukuliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Tamisemi), Hawa Ghasia alipokuwa katika ziara ya siku moja hivi karibuni. Katika ziara hiyo wananchi wa mji wa Kilosa walimlalamikia kutoridhishwa na ujenzi wa barabara hiyo iliyotumia fedha nyingi na ikiwa imeanza kuharibika.

Kwa mujibu wa taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo iliyosomwa na mwakilishi wa Mhandisi wa Ujenzi wa wilaya hiyo, Subira Lukume, barabara hiyo imejengwa na Kampuni ya Deep Construction LTD ya mjini Morogoro , ambapo waziri huyo aliizindua.

Hata hivyo baadhi ya wakazi wa mji huo , akiwemo Juma Bakari pamoja na Godfrey Joseph , walidai tangu ikamilike miezi sita iliyopita na kuanza kutumika lami hiyo imekwishaanza kubanduka na kubakia mchanga hali inayowapa wasiwasi juu ya matumizi mabaya ya fedha za wananchi.

“Nimeizindua barabara hii lakini kabla ya kuizindua nimesikia kumekuwepo na minong’ono ya wananchi kuhusu barabara hii kuwa haijakidhi viwango vya ubora,” alisema Waziri huyo.

Hata hivyo alisema “ ...mimi si mtaalamu wa uhandisi wa kutoa majibu hapa ila nimeagiza wataalamu wa uhandisi kutoka Tamisemi kufuatilia na kukagua ujenzi huu ili majawabu sahihi yapatikane”.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka vijana wa ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Kilosa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi