loader
Hifadhi ya jamii ya NSSF ‘roho kwatu’ Sabasaba

Hifadhi ya jamii ya NSSF ‘roho kwatu’ Sabasaba

Tuzo hizo zilikabidhiwa jana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati wa uzinduzi rasmi wa maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere ‘Sabasaba’, Barabara ya Kilwa.

Washindi wengine katika tuzo hizo ni pamoja na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) katika kundi la kampuni bora za simu, Benki Kuu ya Tanzania katika kundi la mamlaka za udhibiti wa serikali, Wizara ya Maliasili na Utalii katika kundi la wizara bora za serikali.

Aidha, makundi mengine na washindi kwenye mabano ni, Kikundi bora cha wanawake mkoani (Mtwara), Taasisi ya fedha (Benki ya Uwekezaji TIB), huduma za mafunzo (Chuo Kikuu cha Ardhi), mafuta na gesi (Shirika la Maendeleo ya Mafuta na Petroli).

Wengine ni uendelezaji wa ujuzi (VETA), mtengezaji bora wa bidhaa za ngozi (TM Tittos), mtengenezaji na msambazaji wa nishati (Solar Planet 2005), mtengenezaji wa magari na mashine (GF Trucks & Equipment Ltd), fenicha bora (Magereza), Vifaa bora vya Ujenzi (Property International Ltd), wazalishaji wa kilimo na mifugo (Katani Ltd).

Bidhaa za uhandisi (Nation BKeeping Suppliers Ltd), mzalishaji na msambazaji wa bidhaa za vyakula (S.S Bakhresa Group of Companies), teknolojia ya habari na mawasiliano (Tanzania Network Information Center) na uchapishaji na vyombo vya habari (Umoja wa Mataifa UN).

Aidha, Balozi Iddi aliwataka waandaji wa maonesho hayo kutumia fursa hiyo kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini.

Alisema maonesho hayo yamekuwa na mvuto mkubwa wa kibiashara hivyo kufanya hivyo kutavutia wawekezaji wengine na hivyo kuongeza uchumi wa nchi.

Aidha, aliwashauri wafanyabiashara kuhakikisha wanaweka bidhaa zao katika vifungashio vizuri ili kuweza kupata soko la kimataifa.

“Ongezeko la washiriki ni ishara kuwa maonesho haya yanakidhi viwango vya kimataifa na hivyo ni kipindi muafaka kwa wazalishaji wetu kutangaza bidhaa kwa walaji wa ndani na nje,” alisema Balozi Iddi

foto
Mwandishi: Katuma Masamba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi