loader
Dstv Habarileo  Mobile
Hili la Kagame, Maximo ameona mbali

Hili la Kagame, Maximo ameona mbali

Kutokana na mtazamo wangu huu, ndio maana naunga mkono uamuzi wa Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo kupeleka kikosi kitachosheheni wachezaji wengi wa kikosi cha pili cha timu hiyo.

Hoja hapa iko wazi kwa nyota ambao wana uzoefu wa kutosha wa mashindano ya kimataifa, naamini hawataongeza chochote kutokana na mashindano haya, kwani yanafanyika kimazoea tu na sio zaidi ya hapo.

Kutokana na hilo, ni wazi Marcio Maximo kocha mwenye dhamira ya dhati katika kuendeleza soka la vijana, anaamini mashindano hayo yatakuwa na faida zaidi kwa vijana hao wadogo kuliko wangeenda akina Mbuyu Twite.

Maximo atawaunganisha chipukizi hao wengi na wazoefu wachache na naamini baada ya mashindano hayo kumalizika, hata kama Yanga haitatwaa taji hilo, itakuwa imepata wachezaji kadhaa walioongezeka uzoefu kutokana na kushiriki katika mashindano hayo.

Hoja nyingine hapa na iliyo wazi ni uchache wa mechi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara na uwezekano wa wachezaji chipukizi kupata nafasi kubwa ya kucheza kwenye kikosi cha timu kama Yanga ambacho kinaundwa na nyota wengi wenye uzoefu.

Ndio yatabaki yale yale timu inasajili wachezaji 30, lakini kutokana na uchache wa mechi katika ligi yetu, unakuta wachezaji wengi tu wanamaliza ligi bila hata ya kucheza mechi moja au kucheza kwa uchache sana.

Sasa kama hivyo ndivyo, kwa nini wachezaji hawa chipukizi ambao uwezekano wao wa kupata nafasi kubwa ya kucheza kwenye ligi ni mdogo, wasipelekwe kushiriki kwenye mashindano kama ya Kagame?

Hapa inahitaji fikra pevu kuliona hili hasa kutokana na kuwa tumezoea kuona timu zetu zinashiriki tu mashindano kimazoea bila ya kuwa na malengo makini.

Wachezaji kama Nadir Haroub ‘Cannavaro,’ Kelvin Yondani na wengineo, umri unawatupa mkono na hakuonekani dalili ya kutokea kwa haraka wengine wanaofanana na viwango vyao.

Hapa ni wazi kupelekwa chipukizi Kagame kutaandaa wachezaji mbadala wa nyota hao na kuja kuwa na manufaa ya kimataifa baadaye.

Huwezi kupiga hesabu ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia za Qatar 2022 huku mawazoni kwako bado unawawaza akina Cannavaro, Yondani, Mrisho Ngassa na wengineo ambao muda unawatupa mkono na ni wazi hatutakuwa nao kipindi hicho.

Tusiangalie kushiriki mashindano kimazoea tu bila ya kuwa na mtazamo wa mbali. Hivi wakitokea akina Mbwana Samatta wengine kutokana na mashindano ya Kagame, kuna Mtanzania mwenye nia njema atakayechukia? Ni wazi hakuna.

Katika hili, naamini kabisa Maximo yupo sahihi sana na cha muhimu hapa ni wadau kumuunga mkono katika nia yake hii njema ili yakitokea mashindano

WIKI iliyopita umefanyika uzinduzi wa siku ...

foto
Mwandishi: Clecence Kunambi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi