loader
Dstv Habarileo  Mobile
Hili la Ukawa latosha, sasa ijadiliwe Katiba

Hili la Ukawa latosha, sasa ijadiliwe Katiba

Katika kuelekea vikao hivyo vya Bunge Maalumu, kumekuwa na changamoto mbalimbali zilizojitokeza, ikiwa ni pamoja na kundi linalojiita Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuendelea kususia vikao hivyo kwa sababu mbalimbali.

Kundi hilo linaloundwa na wajumbe wa bunge hilo kutoka vyama vikubwa vya upinzani vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR –Mageuzi na vinginevyo, imekuwa ikisababisha sintofahamu kuhusu upatikanaji wa katiba mpya.

Awamu ya kwanza ya bunge hilo, iliambatana na vituko vya kila aina na iliishia kwa wajumbe wa kundi hilo kutoka nje ya Bunge mpaka vikao hivyo vikiahirishwa.

Kutokana na kitendo hicho cha kususa Bunge, kumekuwa na juhudi mbalimbali zilizofanywa na viongozi wa dini, taasisi na wengineo, kuwasihi wajumbe hao kurejea bungeni bila mfanikio.

Kutokana na hatua hiyo, uongozi wa Bunge Maalumu la Katiba uliunda Kamati ya Maridhiano na kuteua wabunge kutoka pande zote za makundi yanayounda wajumbe wa katiba hiyo ili kuweza kufikia muafaka.

Lakini, katika jambo la kushangaza, wajumbe wanaotoka upande wa kundi hilo lisilo rasmi, hawakujitokeza kushiriki katika kikao hicho cha maridhiano, jambo lililosababisha kutofikiwa kwa muafaka wa tofauti zilizopo.

Jambo la kujiuliza ni nini dhamira hasa ya kundi hilo, kuendelea kususia vikao hivyo vya bunge, bila kutaka majadiliano yeyote? Sasa masuala yao ya msingi, yatajadiliwa vipi, kama hawatakaa na kujadili?.

Kutokana na sintofahamu iliyopo, jamii nzima imejikuta ikiegemea kutaka upande wa Ukawa kurejea bungeni na kuacha kujadili masuala muhimu yaliyopo katika rasimu kwa maendeleo ya nchi.

Ikumbukwe kuwa kabla ya kuanza kwa mchakato huo wa katiba, viongozi hawa ambao ni dhahiri hawaeleweki kwa sasa, wanahitaji nini ili kuendelea kwa mchakato huo na kufikia malengo, walikuwa mstari wa mbele kulalamikia katiba iliyopo.

Mimi naamini kuwa wana-Ukawa wameshasikia maoni na wananchi, kuwataka kurejea bungeni, hivyo ni vyema kujitafakari upya ili kuhakikisha mchakato huo, unaendelea na kufikia malengo yanayotarajiwa.

Hivyo kwa mtazamo wangu, umefika wakati muafaka sasa kuendelea kujadili vipengele vya rasimu na kuwaacha Ukawa wajitafakari wenyewe, kuhusu msimamo wao kwa maendeleo ya taifa na wananchi kwa ujumla.

Jambo la msingi ni kuhakikisha wajumbe wa bunge hilo, kila mmoja anajitafakari ni kwa jinsi gani uwepo wake ndani ya bunge, utasaidia nchi na siyo kuangalia maslahi binafsi na kujadiliana kwa mapana na marefu, kutumia muda wa siku 63 zilizobaki kufikia malengo yaliyopo.

Nawasihi wajumbe kuangalia muda na gharama, zinazotokana na kodi za wananchi zilizotumika katika mchakato huu na kutokubali kupotea bure, bali uzae matunda na kuhakikisha katiba bora inapatikana bila migogoro.

WIKI iliyopita umefanyika uzinduzi wa siku ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi