loader
Dstv Habarileo  Mobile
Idadi ya watalii kufikia milioni 2.3

Idadi ya watalii kufikia milioni 2.3

Hatua hiyo inaenda sambamba na kuboresha masuala mbalimbali, ikiwemo utoaji huduma ambao unalalamikiwa na watalii wengi na kuboresha ulinzi na usalama.

Akifungua Kamati ya Huduma za Watalii (TFC) inayoshirikisha wadau mbalimbali wa kutoa huduma kwa watalii, alisema kwa mwaka jana watalii milioni 1.1 waliingia nchini.

“Hii inaanzia katika hati za kusafiria kwa watoa huduma za usafiri na hoteli, upatikanaji wa chakula na kuboresha miundombinu,” alisema.

Alisema wizara inaandaa utaratibu mpya wa kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wataalamu, wanaoanza kufanya kazi na baadaye ndipo waingie darasani.

Alisema hatua hiyo itaongeza mapato, yatokanayo na utalii. Alisema mwaka jana utalii uliingiza zaidi ya Sh trilioni moja, hivyo kuongeza pato la taifa.

Akizungumzia ulinzi na usalama kwa watalii, Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Diplomasia na Watalii, Benedict Kitarike alisema vitendo vya watalii kuvamiwa nchini, vimekuwa vikipungua kila mwaka.

Kitarike alisema matukio ya uvamizi, hufanywa mara nyingi na madereva teksi, ambao hushirikiana na wavamizi. Alisema Jeshi ya Polisi limetoa elimu kwa madereva hao na limeandaa mikakati kukomesha uvamizi.

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwako

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi