loader
Dstv Habarileo  Mobile
Jaji Mkuu awaonya mawakili

Jaji Mkuu awaonya mawakili

Aliyasema hayo leo katika hafla ya kuwakubalia na kuwasajili mawakili 163 wa kujitegemea katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema idadi hiyo ya mawakili itasaidia kuongeza huduma ya mawakili ambayo wengi wanahitaji huduma hiyo ili wapate haki zao. Aliongeza kuwa wakili anatakiwa kutunza siri za mteja kwani kinachoongelewa na wakili na mteja kinapaswa kuwa faragha hivyo ni lazima mzungumzo yao yalindwe.

“Kuna wengine sio waaminifu, wanatoa mazungumzo ya mteja kwa watu wengine kitendo ambacho si maadili ya uwakili,” alisema Chande.

Alisema si mawakili wote waliosajiliwa, watafanya kazi Dar es Salaam, bali kuna wengine watakwenda katika sehemu nyingine za nchi ili nako huduma ya sheria iweze kupatikana.

Pia, alisema mawakili hao waliosajiliwa, wanatakiwa wajiendeleze kitaaluma ili kupata uelewa utakaowasaidia kwenye kazi zao huku akisisitiza kuwa, kupata uwakili sio mwisho wa kujiendeleza.

“Kama mtaalamu wa sheria lazima ujifunze kwani kila unapojifunza ndio kupata uelewa zaidi,” aliongeza Chande.

WAZIRI wa Nishati, January Makamba ameseme wataalamu wa ...

foto
Mwandishi: Sophia Mwambe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi