loader
Dstv Habarileo  Mobile
Jeshi la Magereza kuchimba madini

Jeshi la Magereza kuchimba madini

Tayari jeshi hilo limeshapata leseni 102 za uchimbaji wa madini ya aina mbalimbali nchini ili liweze kupata fedha za kujiendesha.

Hayo yalisemwa jana na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Minja katika hotuba yake aliyoisoma mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Magereza nchini yaliyohudhuriwa pia na wakuu wa vyombo vya ulinzi na wastaafu wengine wa jeshi hilo.

Alisema jeshi lake linakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwamo ufinyu wa bajeti, miundombinu ya magereza, uhaba na uchakavu wa vyombo vya usafiri na mawasiliano, vitendea kazi, ukosefu wa pembejeo pamoja na msongamano magerezani.

“Katika kukabiliana na changamoto ya ufinyu wa bajeti, Jeshi la Magereza limefanya jitihada mbalimbali ili kuongeza tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu, tumefanyia utafiti maeneo yetu na tayari tumekwisha pata leseni 102 za uchimbaji madini, sasa tunatafuta wawekezaji,” alisema Kamishna Minja.

Alisema leseni hizo ni za uchimbaji wa madini ya ujenzi kama chokaa, mawe, kokoto, mchanga na moram katika maeneo mbalimbali ya Magereza nchini.

Aliongeza kuwa, jeshi hilo linaendelea kuomba leseni nyingine katika maeneo yanayoonekana kuwa na madini.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imepata nmkopo ...

foto
Mwandishi: Regina Kumba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi