loader
Dstv Habarileo  Mobile
Jibu la ukatili dhidi ya wenye ulemavu wa ngozi ni mshikamano

Jibu la ukatili dhidi ya wenye ulemavu wa ngozi ni mshikamano

Inawezekana vyombo vya dola vilifanya kazi yake ipasavyo au jamii ilichangia kwa namna moja katika kupunguza kasi ya vitendo hivyo. Hali inayojitokeza sasa ni kwamba ni kuanza kurudi tena kwa kasi kwa matukio ya ukatili dhidi ya wenzetu wenye ulemavu wa ngozi.

Hali hii inatokana na tukio la kikatili la watu wasio na roho za kibinadamu kumfanyia vitendo vya kinyama mlemavu wa ngozi huko mkoani Tabora, kwa kumkata kiwiko cha mkono wake na kutoweka nacho.

Tena inadaiwa kuwa huyo ni wa pili kufanyiwa vitendo hivyo ndani ya muda usiozidi wiki mbili. Mkazi huyo wa Tabora, Suzana Mvungi wa kijiji cha Buhelele, kata ya Nsimbo wilayani Igunga mkoani Tabora alidaiwa kukatwa kiwiko cha mkono wake na watu wasiojulikana na kutoweka nacho na pia mumewe kuuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kifuani na kichwani wakati akijaribu kumnusuru mkewe.

Matukio kama haya yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika jamii yetu, mengi yakihusishwa na mambo ya kishirikina. Hii inadhihirisha kwa asilimia kubwa kuwa jamii ndiyo inayosababisha kuwepo kwa matukio haya ya kinyama kutokana na imani potofu za kishirikina zilizojengeka miongoni mwao.

Ninachotaka kueleza hapa ni kwamba watu wanaofanya vitendo hivi vya kikatili dhidi ya walemavu hao tunaoishi nao mitaani kwetu na wengine wanafahamika.

Wakati umefika sasa kwa wanajamii wenyewe tuwafichue watu hawa washughulikiwe na vyombo vya dola na sio kuwaficha. Jamii yetu inatakiwa kuwa na dhamira ya dhati na ya kweli katika kushikamana kwa pamoja ili kukabiliana na ukatili huu unaofanywa na watu wachache wenye kukosa utu.

Jamii ikishirikiana kwa dhati na vyombo vya dola kutakuwapo na uwezekano mkubwa wa kuwatia mbaroni kisha kuwafikisha katika vyombo stahiki waweze kupata wanachostahili kwa vitendo hivyo viovu ndani ya jamii yetu.

Kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu katika jamii zetu kufadhili makundi ya wahalifu kwa masilahi yao binafsi, watu hao tunao tunaishi nao kwa nini wasianikwe hadharani ili washughulikiwe badala kuilaumu serikali kwa mfano?

Kwa suala hili narudia tusimtafute mchawi na badala yake tukabiliane na majahili hao ili kulinda utu na heshima ya taifa letu ambalo kwa kweli linasifika barani kwetu na duniani kwa ujumla kwa amani, utulivu, umoja na mshikamano.

Nani asiyejua kwamba Tanzania imekuwa kimbilio la wengi waliokuwa na matatizo ya kisiasa wakati wa kupigania uhuru katika nchi mbalimbali za Afrika.

Nani asiyejua kwamba nchi jirani zimekuwa zikipata hifadhi nchini Tanzania kutokana na madhila wanayopata katika nchi zao? Tusikubali kudhalilishwa na kundi hili dogo lenye uchu wa ajabu bali tudhamirie kuwadhibiti na kuwatokomeza ipasavyo kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

TANESCO ni shirika la huduma lakini pia ni ...

foto
Mwandishi: Fadhili Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi