loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DIMBWI LA MAHABA: Jinsi ya kudhibiti hasira kwenye uhusiano

Pamoja na ukweli huo, zipo njia thabiti zinazoweza kukusaidia kuepuka kuacha hasira zako kukufanya uonekane mtu wa ajabu mbele ya mwenza wako na hata kufikia hatua ya kukuharibia uhusiano wako.

Athari za kuendekeza na kushindwa kudhibiti hasira zako ni kubwa na wakati mwingine zinaweza kukufanya watu wakakaa mbali na wewe na kushindwa hata kujaribu kutafuta suluhu ya tatizo.

Wapo watu kwenye uhusiano hutumia udhaifu huo wa hasira, pindi wanapokorofishana na wenza wao, na kuamua kuchukua hata wiki wamenuna, visirani na wakati mwingine hata kutoa maneno yasiyo na staha.

Ukweli ni kwamba, ule usemi usemao hasira hasara, haujakosea hata kidogo, endapo mtu atashindwa kudhibiti hasira zake akiwa na mwenza wake, kuna hatari ya kufanya mambo mabaya ambayo baadaye baada ya hasira kushuka kujikuta anajuta.

Ingawa ni kweli si rahisi nyakati zote kudhibiti hisia zako, lakini unaweza kudhibiti maneno na matendo yako. Hakuna haja ya kulipuka kwa hasira pindi mwenza wako anapokosea au inapotokea tofauti kati yenu. Jambo la msingi ni kuhakikisha kila mmoja wenu anajifunza namna ya kujidhibiti anapokasirishwa.

Kama jambo limekuudhi kupita kiasi, badala ya kufoka, kupiga kelele hadi wakati mwingine majirani wanasikia, jaribu kutuliza kwanza akili yako kwa kujipa muda wa kuvuta pumzi ndipo useme unachotaka kusema.

Usithubutu kuacha hisia na hasira zako zikutawale kwani hizo ndio hukusababishia kufanya mambo ya ajabu kama vile kuvunja vitu, kutukana, kukejeli au kuamua tu kununa bila kutafuta suluhu ya tatizo.

Aidha ni vyema ukajipa muda na kutafakari kwani wakati mwingine huenda umekasirika kwa sababu ya kufikiria upande mmoja tu wa jambo lililokupata, yaani, sehemu iliyokukasirisha wewe.

Jitahidi pia kuelewa jinsi mwenza wako naye anavyohisi. Hata hivyo, washauri wa masuala ya saikolojia ya uhusiano wanadai kuwa endapo wenza wakiona ugomvi kati yao umekuwa mkubwa na hakuna maelewano, ni vyema mmoja wao akaondoka eneo husika ili kutoa muda kwa kila mmoja wao kutafakari juu ya kilichotokea.

Tiba njema inapotokea tatizo kama hilo ni kupeana na muda na baada ya kila mmoja kutuliza hasira na hisia zake kuhusu kilichotokea, mnaweza kuzungumzia tatizo kwa pamoja na kulitafutia ufumbuzi kwa utulivu bila kukwaruzana.

HAKUNA siri kila mtu anatamani sura nzuri na rangi isiyo ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi