loader
Juhudi zaidi zatakiwa kuitangaza Serengeti

Juhudi zaidi zatakiwa kuitangaza Serengeti

Kauli hiyo ilitolewa jana na Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Serengeti, Sethi Mihayo.

Alisema kwa sasa baadhi ya vyombo vya habari vya nchi jirani vimekuwa vikitangaza kuwa hifadhi hiyo iko nchini Kenya na inaitwa Masai Mara Serengeti.

Alisema upotoshwaji huo wa makusudi unapaswa kubainishwa kwa kuongeza kasi ya kujitangaza.

Alisema kazi ya kukanusha upotoshaji huo inapaswa kufanywa na kila mtanzania mwenye nia njema na nchi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bodi ya Utalii na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ili watalii waweze kujua ukweli halisi na sio kuyumbishwa na vyombo hivyo.

UJENZI  na ukarabati wa Soko la Kariakoo jijini ...

foto
Mwandishi: Na John Mhala, Serengeti

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi