loader
JWTZ yaombwa paa uwanjani Migombani

JWTZ yaombwa paa uwanjani Migombani

Ombi hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili na Utamaduni Jeshini, Luteni Kanali Joseph Bakari alipotoa maelezo katika uzinduzi wa uwanja huo ambao ulizinduliwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange.

Luteni Kanali Bakari alisema uwanja huo ambao utatumika kwa michezo minne, ikiwemo mpira wa kikapu, mikono, wavu na netiboli, umejengwa kwa viwango vya kimataifa.

“Uwanja huu ili uweze kudumu na kukamilika lengo lake la kuwa ni kiwanja cha michezo ya ndani tunaomba uwanja huu uwekewe paa ili kuwa madhubuti,” alisema.

Katika uzinduzi wa uwanja huo kulifanyika mchezo maalumu uliowakutanisha Kombaini ya Vikosi vya SMZ na Kombaini ya JWTZ ambao ulimalizika kwa JWTZ kushinda mabao 25-21.

Uwanja huo ulioanza kujengwa Juni 6, mwaka huu na kukamilika Agosti 8, mwaka huu, una majukwaa mawili ambayo yote kwa pamoja yana uwezo wa kuchukua watu 100.

SIMBA Queens imekuwa timu ya ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi