loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

KAMA MZAZI: Tukatae kuzalisha vilema kwa jeuri ya bodaboda

Hakuna ubishi kwamba idadi kubwa ya madereva wa bodaboda ni vijana wa chini ya miaka 20 ambao wengi wao huwakuwahi kupata mafunzo yanayostahiki kuendesha vyombo vya moto barabarani na hivyo wakati mwingine kukiuka sheria kwa kutojua tu na kuhatarisha maisha yake na abiria anaowachukua.

Madereva hao labda ni kutokana na umri wao huendesha kwa mwendo kasi, kuyapita magari upande wowote ule iwe kulia au kushoto ilimradi ipite. Yaani eti wanaona ni kero kwa watumiaji wengine wa barabara hata waenda kwa miguu kama vile wanawachelewesha kuwahi wateja wao.

Bodaboda akifika kwenye eneo lenye mataa, hata kama zinamwonesha taa nyekundu inayomtaka asimame, hilo huliona halimhusu na hivyo kuendelea kutafuta mwanya wa kupenya. Wengi wanapenya na kuendelea na safari huku wakati mwingine polisi wakiwashuhudia bila kuchukua hatua dhidi yao.

Ni kama vile sheria ya usalama barabarani wao haiwahusu kabisa ni kwa wengine tu. Taarifa ya Jeshi la Polisi wa Usalama Barabarani kwa mwaka jana 2016, ilionesha kuwa ajali za bodaboda zilisababisha vifo vya watu 820 na majeruhi 1,998.

Kutokana na takwimu hizo wapo walioachwa yatima, wajane na wagane huku familia nyingine zikiwa zinabakiwa na majeruhi ambao ni tegemezi kutokana na ulemavu waliopata kwa ajali za bodaboda. Viroba navyo havikukosekana kwenye mifuko ya madereva wa bodaboda na ni vyema sana serikali ilivyofanya kwa kuvipiga marufuku.

Bila shaka hatua hiyo itakuwa imesaidia kupunguza tatizo. Kama kwa mwaka jana peke yake waliojeruhiwa walikaribia 2,000 hivi kasi ikiendelea hivi, ifikapo miaka 10 ijayo au zaidi, tutakuwa tumetengeneza vilema wangapi?

Tujikumbushe kwamba bodaboda ziko kwenye ngazi za miji, wilaya, manispaa, mikoa na majiji, kwa kasi hii tutakuwa tunazalisha vilema wangapi kwa mwaka? Kwa nini polisi kwa kushirikiana na wamiliki wa vyombo hivyo na wazazi wasipange mikakati ya makusudi kukabiliana na janga hili la wazi kabisa kwa kuhakikisha kwamba madereva hao wanapewa mafunzo ya muhumu ya uendeshaji wa bodaboda na kupewa leseni kwanza kabla ya kujikita moja kwa moja kwenye udereva huo?

Kama wenye magari na vyombo vingine vya moto hawaruhusiwi kuwa barabarani mpaka wawe wamepata mafunzo stahiki na kupewa leseni kwa ajili ya kazi hiyo, kinachokwamisha mafunzo kama hayo yasifanyike kwa madereva wa bodaboda ni nini?

Kama Mzazi inasema kwa dhati juu ya hili kwamba asitafutwe mchawi ni nani kwani jambo ambalo liko wazi na likichukuliwa hatua za kukabiliano nalo moja kwamoja, tutaokoa maisha ya watanzania na kupunguza mzigo wa vilema tegemezi. Tusikubali kuishi na janga hili, bali hatua zichukuliwe kulikabili.

HAKUNA siri kila mtu anatamani sura nzuri na rangi isiyo ...

foto
Mwandishi: Nicodemus Ikonko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi