loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

KAMA MZAZI: Utandawazi na malezi ni jino kwa jino

Hiki ni kizazi cha matumizi mkubwa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kupitia kompyuta, simu za mkononi, mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na barua pepe, tovuti, Facebook, YouTube na mingine mingi.

Tofauti na wakati wa analogia ambapo ili kuwasiliana tulihitaji kuandikiana barua, kutumia telegramu za ujumbe mfupi au fedha kwa njia ya mitandao ya posta au kwa njia ya simu zilizounganishwa nyaya na kuchukua muda mrefu kabla ya mhusika kupata ujumbe.

Hali hiyo sasa inaendelea kukaribia kuwa historia kwa maana ya matumizi yake yanazidi kupungua kutokana na uvumbuzi na maendeleo ya ICT. Mawasiliano sasa yapo kiganjani mwako.

Unachohitaji ni kuwa na simu yako ya mkononi yenye uwezo wa kupokea huduma hizo mara moja toka mahali ulipo mradi mahali hapo pawe ni mtandao unakuwezesha kukuunganisha na wengine mahali popote.

Unaweza kusikikia radio, kushuhudia matukio yanayotangazwa moja kwa moja na televisheni na radio mahali popote duniani au hata kusoma magazeti kwenye mitandao bila kulazimika kwenda kulinunua mahali.

Mawasiliano ya dijitali yanavuka mipaka ya nchi na mabara duniani. Unatuma ujumbe sasa hivi kwa kutumia mitandao na katika kipindi cha karibu chini ya dakika moja mamia, maelfu na pingine mamilioni ya watu wanaweza kushuhudia duniani.

Lakini urahisi huu wa mawasiliano sasa nao umekuja na mfumo hasi pia katika suala zima la malezi ya watoto. Udhibiti wa mienendo yao, au aina ya taarifa wanazotafuta kupitia mitandaoni na picha au matukio wanayostahili kuyaona watoto wa chini ya miaka 18 sasa yanaelekea kuwa ndoto za mchana kuweza kuyadhibiti.

Watoto hivi sasa kwa kweli wako katika dunia ya utandawazi kiasi kwamba wazazi na walezi makini tupo katika njia panda. Tufanyeji ili tuweze kurejesha angalau kwa kiasi fulani udhibiti wa tabia na maisha yao kama watoto, tena watoto wa kiafrika?

Ni kama vile undawazi umeshafikia hatua za kutuzidi nguvu wazazi na udhibiti wa tabia hasa wanazojifunza watoto kupia utandawazi. Watoto wetu hata kama hatuwanunulii simu za kuweza kufanya mawasiliano wanayopenda, huweza kutumia simu za marafiki zao au kwenda kwenye vioski vya mitandao kubrauzi wenyewe na kujipatia picha za ajabu ajabu zikiwemo za ngono.

Zamani wakati wa analogia wazazi waliweza kutoka na watoto wao kwenda kwenye majumba ya sinema zinazoonesha picha ambazo watu wazima na watoto kwa pamoja wanaweza kuziona.

Hivi sasa majumba hayo hayapo kwa uwingi kama wakati wa enzi hizo. Utandawazi umeathiri na kuendelea kuathiri watoto wetu kwa kupitia simu za kiganjani, televisheni, muziki wa kizazi kipya, sinema za ngono na wala siyo mapenzi kiasi kwamba watoto wetu tumewajengea taswira kwamba dunia hii ni raha na starehe tupu. Tutafika kweli?

MENO meupe na safi ni moja ya vitu vinavyoongeza mvuto ...

foto
Mwandishi: Nicodemus Ikonko

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi