loader
Kampuni 9 za mafuta zafutiwa leseni

Kampuni 9 za mafuta zafutiwa leseni

Uamzi huo ulifanywa jana katika kikao cha Bodi ya Wakurugenzi kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Ewura, Simon Sayore kutokana na kampuni hizo kukiuka masharti ya biashara.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi, kufutwa kwa leseni hizo, kumetokana na ukiukaji wa sheria na kanuni za biashara hiyo.

Ngamlagosi katika taarifa yake, alisema kampuni hizo zimefutiwa leseni kutokana na kukaa bila kuagiza mafuta kama leseni inavyowataka kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita tangu kupewa leseni hizo na Ewura.

Kampuni zilizofutiwa leseni ni Aspam Energy (T) Limited, MPS Oil Tanzania Limited, Panone Bulk Oil Importers Limited, Petcom (T) Limited, KMJ Tanzania Limited, Horizon Petroleum Company Limited, G.M and Company (T) Limited na Petronas Energy Tanzania Limited.

Mamlaka hiyo imeundwa chini ya sheria ya Ewura Sura Namba 414 ya Sheria za Tanzania. Mamlaka hiyo ina majukumu ya kusimamia shughuli za udhibiti, kiufundi na kiuchumi katika sekta za Petroli, Umeme, Gasi Asili na Maji Safi na Maji Taka.

Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Misaada la taifa hilo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi