loader
Kampuni kushindana Reli ya Kati

Kampuni kushindana Reli ya Kati

Imeelezwa kwamba serikali itakapokamilisha treni za kutosha na kuongeza wafanyakazi ambao wataweza kujitegemea, wataingia katika ushindani wa kibiashara na kampuni binafsi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, alipozungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Reli (TRL) kuhusu mikakati ya kutimiza mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Alisema watahakikisha kampuni binafsi zinalipa ushuru watakapotumia usafiri wa Reli ya Kati, kuongeza ufanisi katika reli hizo.

Alisema watakapowaandaa wafanyakazi kukabiliana na ushindani kutoka kampuni binafsi, itasaidia kuondoa ubadhirifu miongoni mwa wafanyakazi hasa wizi wa mafuta.

Aidha, alisema Jumamosi treni zitaanza kusafirisha mizigo kwa kutumia reli ya kati kwa Mikoa ya Kigoma, Mwanza na Isaka.

Alisema tayari vipo vichwa vitano vya treni na mabehewa 60 ambayo yataanza safari katika mikoa hiyo. Pia vichwa 21 na mabehewa 200 yanayokarabatiwa yanatarajiwa kumalizika Agosti mwaka huu.

WADAU wa Sekta ya Kilimo nchini wameshauriwa ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi