loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kampuni za madini Mbeya zabanwa

Kampuni za madini Mbeya zabanwa

Maswi alitoa agizo hilo mjini Mbeya jana, wakati akizungumza na wafanyakazi wa Idara ya Madini mkoani Mbeya, ambako alipatiwa taarifa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), kuhusu kampuni kubwa tatu zinazogoma kulipa maduhuli stahiki kwa Serikali, kwa madai ya kuwa na hati ya msamaha wa kodi katika baadhi ya maeneo.

“Hili jambo mbona ni rahisi kwa kuwa sekta yetu hii ya madini inaendeshwa kwa kuzingatia sheria, na sheria inatamka wazi kuwa ni lazima kila mwekezaji wa madini alipe maduhuli kulingana na kiasi alichouza.

“Kamishna wa Madini fuatilia hili na kama kweli kuna hizo hati…kwani zinatoka wapi? Si zimetoka serikalini basi zifutwe, hawa walipe malipo stahiki,” alisisitiza Maswi.

Awali akiwasilisha ripoti ya ukaguzi wa TMAA katika Mkoa wa Mbeya, Ofisa Mfawidhi wa wakala huo mkoani hapa, Jumanne Abdallah, alisema ofisi yake imekuwa ikikabiliwa na wakati mgumu katika ukusanyaji wa maduhuli kutoka kampuni hizo za madini na kushindwa kukusanya malipo stahiki.

Alisema kwa mujibu wa sheria hiyo, kampuni hizo zilitakiwa kulipa Sh milioni nne kwa mwezi kodi ya maduhuli, lakini kutokana na madai ya kuwa na hati hizo, zimekuwa zikilipa kila mwezi Sh milioni 3.

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha, Kiwira

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi