loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kibaha Vijijini kuchagua timu ya Copa Coca-Cola

Kibaha Vijijini kuchagua timu ya Copa Coca-Cola

Mashindano hayo yatafanyika ili kutekeleza agizo la Chama cha Soka Mkoa wa Pwani (COREFA), ambapo mchujo wa mwisho utafanyika Agosti 16, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mashindano wa KIVIFA, Mohamed Msamati alisema tayari wameshakaa na klabu 11 ili kuwaelekeza namna ya kufanya mashindano hayo.

Msamati alisema kwa sasa wako kwenye maandalizi ya michuano hiyo ambayo itashirikisha timu zote za Kibaha Vijijini na kuzitaka timu kujiandaa na mashindano.

“Kila timu inapaswa kuandaa wachezaji wake kwa kufanya mazoezi ya kutosha ili kuhakikisha wilaya inapata wachezaji wazuri watakaowakilisha kwenye mashindano ya mkoa,” alisema Msamati.

Aidha, alisema watahakikisha mashindano hayo yanatumia wachezaji ambao wana umri unaopaswa na kuepukana na kutumia wachezaji ambao wana umri mkubwa maarufu kama vijeba.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa KIVIFA, Meja mstaafu Deus Makwaya alisema wamejipanga vizuri katika kuhakikisha mashindano hayo yanafanikiwa na kupata timu bora.

Meja Makwaya alisema tayari wameteua viongozi kwa ajili ya kusimamia mashindano hayo ya Copa Cola Cola ambao ni Dk Musa Sama ambaye ni Mwenyekiti, Juma Likali Katibu na God Mwafulilwa Meneja.

Aliwataja wajumbe kuwa ni Hija Matitu, Juma Kisebengo, Said Kidile huku walimu wakiwa ni Said Shaban na Mtoso ambao ni timu ya ushindi ya kuandaa vijana hao.

YANGA leo saa 1:00 usiku itashuka dimbani kuikabili ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi