loader
Kigoda ahimiza uendelezaji wa viwanda

Kigoda ahimiza uendelezaji wa viwanda

Waziri wa Wizara hiyo, Dk Abdallah Kigoda alisema hayo Dar es Salaam jana katika Wiki ya Utumishi wa Umma na kuongeza kuwa ipo haja ya kuimarisha mazingira wezeshi ya uwekezaji.

“Azma yetu ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati hatuwezi kuikamilisha kama hatuwezi kuelekeza nguvu katika viwanda vidogo…ni vyema kutekelezwa hali hiyo ili kupunguza gharama za kuanzisha biashara nchini,” alisema Dk Kigoda.

Alisema kwa utaratibu huo ndipo Tanzania itaweza kupambana na udikteta wa uchumi unaoendelea kusumbua nchi changa duniani ikiwemo Tanzania.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Janeth Mbene alisema Tanzania inatakiwa kuondokana na utegemezi mkubwa wa mapato kutokana na uzalishaji wa bidhaa ambazo hazijaongezewa thamani.

Alisema ipo haja ya kuanzishwa viwanda vingi, vinavyotumia rasilimali zilizopo nchini ili kuuza nje mazao na bidhaa zilizosindikwa na kuongezewa thamani pamoja na kurasimisha sekta isiyo rasmi, ambayo ni kubwa.

Mbene alisema kufanya hivyo, kutaongeza ajira, mapato na kukuza uchumi.

Alisema kinachotakiwa kufanywa ni kuwekwa kwa msukumo kwenye maeneo ya tija kubwa ili kuhudumia yale yanayokuwa na tija ndogo ili kupunguza pengo la ukuaji wa uchumi nchini.

AS Tanzania celebrates its 60th anniversary of independence on ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi