loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kikwete akusudia kuwa mhadhiri

Kikwete akusudia kuwa mhadhiri

Rais Kikwete alisema hayo jana mchana wakati alipotoa Mhadhara kuhusu Usalama wa Taifa, mbele ya wanafunzi wa Chuo hicho kilichoko Kunduchi.

Aliwaambia wanafunzi wa kozi ya pili ya chuo hicho kutoka nchini na nchi za jirani za Uganda, Kenya na Rwanda;

“Najisikia mwenye raha sana kuweza kurudi darasani kutoa mhadhara huu. Tukio hili linanikumbusha enzi zangu katika Chuo cha Kijeshi cha Monduli (TMA). Ni matarajio yangu pia kuwa nitaweza kurudi kuwa mhadhiri katika chuo hiki baada ya kukamilisha kazi yangu ya sasa.”

Rais Kikwete ambaye alizungumza kwa kiasi cha saa mbili, alianza mhadhara wake baada ya kupata maelezo kuhusu maendeleo ya chuo hicho na baadaye akajibu maswali ya wanafunzi, ambao walimuuliza kuhusu mambo mbalimbali yanayohusiana na usalama wa nchi.

NDC ilianzishwa rasmi Septemba 2, mwaka 2012 na chuo hicho kilizinduliwa na Rais Kikwete Septemba 10, mwaka huo huo, 2012 wakati alipotembelea chuo hicho kwa mara ya kwanza, kufuatia juhudi kubwa za uongozi wake kuhakikisha kuwa chuo cha namna hiyo na cha aina yake kinaanzishwa nchini.

Rais pia alifungua kozi ya kwanza ya chuo hicho. Kundi la wanafunzi wa kwanza kwenye chuo hicho, lilimaliza mafunzo yake Julai 23, mwaka 2013 na sasa chuo hicho kinaendesha kozi ya pili yenye wanafunzi 30.

Chuo hicho tayari kimepata usajili kamili wa NECTA, ambako kina uwezo wa kutoa shahada ya uzamili katika masomo ya Strategic Studies (Taaluma za Mikakati).

HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imepata nmkopo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi