loader
Kili Music Tour yapeleka uhondo Kigoma kesho

Kili Music Tour yapeleka uhondo Kigoma kesho

Hili ni onesho la tatu katika awamu ya pili ya ziara hiyo ambayo imezoa umaarufu mkubwa miongoni mwa mashabiki wa muziki nchini kutokana na umaarufu wa wasanii wanaohusika.

Tamasha la Kigoma litafanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika leo ambako wananchi wa Kigoma wana matarajio makubwa kutokana na mambo waliyoyasikia kutoka mikoa mingine.

“Ziara hii ina lengo la kuwapeleka wasanii kwa wananchi na pia ina lengo la kukuza muziki wetu wa ndani ndio maana tulichagua kaulimbiu ya kikwetu kwetu yaani tunajivunia kilicho chetu,” alisema Meneja wa Bia ya Kilimanajro Premium Lager, George Kavishe.

Aliwaomba wakazi wa Kigoma wajitokeze kwa wingi wawaone wasanii wao na pia wapate burudani ambayo wameikosa kwa muda mrefu.

Alisema kiingilio katika tamasha hilo ni Sh 3,000 na kila anayeingia atapata bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kwa wenye umri wa miaka 18.

Wasanii wanaotarajiwa kutoa burudani ni Diamond, Profesa J, Weusi, Ben Pol, Mzee Yusuph, Mwasiti, Mwana FA, Amini na Christian Bella.

Ziara hiyo inaratibiwa na East Africa Tv and Radio, Executive Solutions, Aggrey and Clifford, Integrated Communications na Aim Group. Baada ya Kigoma, ziara hiyo itakwenda Tanga na baada ya hapo itafanya onesho kubwa Dar es Salaam Septemba 6, ikiwa ni funga kazi.

SIMBA Queens imekuwa timu ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi