loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kituo cha kuuza madini ya vito kujengwa

Kituo cha kuuza madini ya vito kujengwa

Kamishna wa Madini nchini, Paul Masanja aliyasema hayo mjini hapa jana wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na wizara yake.

Maswi, ambaye alisema lipo ongezeko la hazina ya madini hayo nchini, alisema kituo hicho kitakuwa na huduma zote muhimu zikiwemo za kibenki zitakazowawezesha wachimbaji na wafanyabiashara kutokutafuta huduma muhimu zinazoendana na shughuli hizo nje ya kituo hicho.

“Shughuli zote za uuzaji na ununuzi madini ya vito na usonara zitafanywa katika kituo hicho, kutakuwa pia na helkopta itakayotua moja kwa moja katika jengo hilo jambo ambalo litawezesha uwepo wa usalama katika biashara nzima ya kuuza na kununua madini.

“Tunataka kupitia sekta ya madini kuiwezesha serikali kuongeza mapato yake na kutoka hapa tulipo kiuchumi.

“Jambo hilo linawezekana ndio sababu tunaanza na kuboresha sehemu za kazi ili kuwawezesha watumishi kufanya kazi katika mazingira mazuri zaidi na kuongeza uwajibikaji,” alisisitiza Masanja.

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha, Songea

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi