loader
Kituo cha Tanzania, Burundi kuanza mwezi huu

Kituo cha Tanzania, Burundi kuanza mwezi huu

Kituo hicho kilichoko eneo la Kabanga nchini na Kobero nchini Burundi, kitasaidia uvukaji wa abiria na usafirishaji wa bidhaa.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Vedastina Justinian alisema hayo jana katika Maonesho ya 38 Biashara ya Kimataifa.

Alisema matumizi ya vituo hivyo vya pamoja, yatafanya msafiri kukaguliwa sehemu moja ya anakoelekea, huku idara zote zikiwa katika jengo moja.

“Kuanza kwa kituo hiki, kutasaidia katika kuweza kuangalia changamoto mbalimbali zitakazojitokeza ili kuzifanyia kazi, ingawa hatutegemei changamoto kubwa kutokana na kuwa mfumo huu wa vituo vya pamoja unafanyika katika nchi nyingi,” alisema.

Justinian alisema vituo vingine vya pamoja vya Holili/Taveta, Sirari /Isebania, Namanga, Rusumo, Horohoro/Lungalunga vimefikia katika hatua mbalimbali kukamilika.

Vingine ambavyo haviko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kama Tunduma/Nakonde mpakani mwa Zambia, Kasumulu/Songwe mpakani na Malawi na Mtambaswala mpakani na Msumbiji, vinatarajia kuanza kujengwa mwaka huu.

Alisema vituo hivyo vya pamoja, vitadhibiti na kuboresha utoaji huduma za kiforodha na uhamiaji kwa ushirikiano na ufanisi zaidi, hivyo kukuza biashara, uwekezaji, uzalishaji na usafirishaji.

WAKALA wa Usafi ri wa Mabasi ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko na Katuma Masamba

Post your comments