loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kituo cha Ubungo chageuzwa soko

Kituo cha Ubungo chageuzwa soko

Hatua hiyo imetokana na ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka ambao umesababisha kutotumika tena.

Wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali ikiwemo mitumba, mboga na matunda, ndiyo wamechukua nafasi kwa kutandaza bidhaa zao kwenye njia zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kushusha na kupakia abiria.

Daladala ambazo zimeonekana kwenye kituo hicho, ni zile zinazofanya safari zake nje ya Dar es Salaam; zinazokwenda Kibaha, Mlandizi na Msata; ambazo hata hivyo hupata shida wakati wa kuingia na kutoka kutokana na ujenzi kuathiri njia.

Kwa upande wa daladala zilizokuwa zikiingia ndani ya kituo hicho cha Ubungo kutoka Mbagala, Temeke, Tandika, Tabata na Gongo la Mboto, kwa sasa zinapakia na kushusha abiria kando ya barabara ya Mandela mkabala ya mitambo ya Tanesco.

Aidha daladala zilizokuwa zikitoka Posta, Kariakoo, Masaki na Mwananyamala kupitia barabara ya Morogoro, huishia njiani. Kwa upande wa zinazokwenda Kimara, Mbezi na Kibamba, zinapakia nje ya kituo hicho.

Akizungumzia uwepo wa masoko yasiyo rasmi katika maeneo mbalimbali, Msemaji wa Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Mhowera alisema wataendelea na operesheni zao kila mwezi kuwaondoa wafanyabiashara husika.

Hata hivyo alisisitiza wananchi kuacha kununua bidhaa katika masoko yaliyopigwa marufuku ikiwa ni njia mojawapo ya kuwafanya wafanyabiashara husika waondoke.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imepata nmkopo ...

foto
Mwandishi: Sophia Mwambe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi