loader
Kiwanda cha TANICA kukusanya bil.6.5/-

Kiwanda cha TANICA kukusanya bil.6.5/-

Kahawa hiyo iliuzwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2013 hadi Aprili 30 mwaka huu. Meneja Mkuu wa Tanica, Leonidas Nshansha alisema hayo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi.

Alisema malengo ya kampuni hiyo tangu Mei Mosi mwaka jana yalikuwa ni kuzalisha tani 255 za kahawa ya unga na tani 270 za kahawa ya kukaanga.

Alisema hadi sasa kiwanda kimezalisha tani 251 za kahawa ya unga na kahawa ya kukaanga uzalishaji wake unaendelea kwa asilimia 100. Nshansha alisema kuwa kipindi cha mwaka wa fedha unaokaribia kuisha, malengo yanaweza kukamilika kwa kiasi kikubwa, tofauti na mwaka 2012.

Mwaka huu mafanikio yataongezeka, japo haijajulikana ni faida kiasi gani watapata ukaguzi utakapofanyika baada ya kufunga mahesabu ya mwaka.

Pia alisema kutokana na kuwepo changamoto hasa katika soko la dunia, hususan uwepo wa bei isiyokidhi gharama za uzalishaji, kampuni hiyo imejiimarisha katika soko la ndani, kwa kutoa kipaumbele kwa watumiaji wakubwa wa kahawa hiyo katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Dodoma, Kigoma, Katavi na Rukwa.

Pia, kampuni imeendelea kujiimarisha katika soko la Afrika Mashariki, hasa Kenya, ambayo ndiyo nchi inayoongoza kwa kutumia kahawa.

foto
Mwandishi: Angela Sebastian, Bukoba

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi