loader
Kova ahimiza bodaboda kujiunga na Saccos

Kova ahimiza bodaboda kujiunga na Saccos

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alitoa ushauri huo mwishoni mwa wiki wakati akizindua pikipiki mpya aina ya Hero Dawn 125cc katika hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya Astarc.

Kova alisema endapo waendesha bodaboda, watajiunga katika vikundi, itakuwa rahisi kwao kuaminiwa katika sekta za fedha na hivyo kunufaika na mikopo.

“Nataka tuirudishe kazi ya bodaboda kuwa kazi ya heshima, jiepusheni na vitendo vya uhalifu ili kazi yenu iweze kupata heshima na jamii iweze kuwaamini”, alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Astarc ambayo ni wakala wa Kampuni ya Hero Motocorp ya India nchini inayotengeneza pikipiki hizo, Sameer Musale alisema aina hiyo ya pikipiki ni mkombozi kiuchumi kwa bodaboda.

Kwa mujibu wake, imetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu inayomwezesha mtumiaji kuendesha zaidi ya kilometa 65 kwa kutumia lita moja ya mafuta ya petroli.

Alisema kampuni hiyo ya India wanauza zaidi ya pikipiki milioni sita kwa mwaka .

“Hero Dawn 125cc imetengenezwa maalumu kwa mahitaji ya Tanzania na inafungwa hapahapa lengo letu ikiwa ni kuinua maisha na pia kusaidia kuongeza ajira kwa vijana wa Tanzania”, alisema.

Wakati huo huo, akitaja takwimu kuhusu ajali zilizowahusisha bodaboda, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi, alisema kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Mei, 2013 jumla ajali 380 zilitokea na kusababisha vifo 11 na kuacha majeruhi 350.

“Natoa wito kwa madereva wa bodaboda kuendesha pikipiki zenu kwa umahiri na kufuata sheria zote za barabarani ili kupunguza idadi ya ajali zinazoongezeka kila siku”, aliongeza.

WAKALA wa Usafi ri wa Mabasi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi