loader
Leo ni leo Miss Kanda Temeke

Leo ni leo Miss Kanda Temeke

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa BMP Promotions, Benny Kisaka, alisema shindano hilo litafanyika kwenye Ukumbi wa Klabu ya Sigara, Chang’ombe, ambapo warembo watatu wa kwanza watapata tiketi ya moja kwa moja kushiriki shindano la Taifa la Miss Tanzania litakalofanyika baadaye mwaka huu.

Kisaka alisema taji linaloshikiliwa na mrembo kutoka Kanda ya Kati, Temeke imejizatiti kutoa si tu Miss Tanzania, bali warembo watatu wa kwanza wa Taifa kutokana na viwango vya warembo wa mwakahuu.

“Kulifanyika shindano dogo la awali lililoandaliwa na Michuzi Media la Miss Photogenic ambalo mshindi wake atazawadiwa kitita cha shilingi milioni moja taslimu, shindano ambalo lilisimamiwa na jopo la wapigapicha wa kampuni hiyo ambao watamtangaza na kumpa zawadi mshindi siku ya shindano,” alisema.

Kisaka aliwataja warembo wanaotarajiwa kupanda jukwaani kuwa ni Subira Ally, Hellen Yughin, Catherine Alex, Dalina David, Winfrida Guntram, Salama Salehe, Grace John, Lilian Lothy, Amina Salim, Rebecca Mdamu.

Wengine ni Sitti Mtemvu, Hellen Sule, Neema Mollel, Lucy Lewis, Esther Mnahi, Pauline Nkini na Patricia Ponsian, waliokuwa chini ya ukufunzi wa Super Bokilo, Shadya Mohamed na Sweet Remmy.

Alisema nyota wa muziki wa kizazi kipya, Khalid Mohamed ‘TID’ na Wanne Star, Makirikiri wa Tanzania na wasanii wengine watapamba shoo.

SIMBA Queens imekuwa timu ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi