loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Luizio kutua Dar na Zesco

Luizio kwa sasa ni mchezaji wa Zesco baada ya kufuzu majaribio hivi karibuni na kwa mujibu wa Meneja wa timu hiyo, Mabvuto Banda, ni mchezaji wao ila hakupenda kueleza amesaini kwa muda gani.

Banda na Ofisa Tawala wa timu hiyo, Franco Chitambala wako Dar es Saalam tangu juzi ili kuangalia sehemu ambako watafikia wachezaji.

Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo, Banda alisema anashukuru kualikwa na Simba kwenye tamasha hilo kwani ni sehemu ya kujenga mahusiano bora.

“Kikosi chetu kitatua kesho (leo), tumefurahi kuchaguliwa kwa sababu katika bara letu la Afrika kuna timu nyingi, tutacheza vizuri,” alisema Banda.

Makamu wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ alisema jana kuwa kikosi kiko vizuri na kinaendelea na mazoezi katika kambi ya Kunduchi wakati wakijifua kwenye Uwanja wa Boko nje kidogo ya Jiji.

Kiungo Jonas Mkude hatakuwepo kwa vile bado ni majeruhi, lakini anaendelea vizuri na siku za karibuni atajiunga kambini tayari kuitumikia msimu ujao.

“Uwanja wa Taifa utafunguliwa kuanzia saa nne asubuhi ambapo tutaanza kuuza tiketi kwa kiingilio cha Shilingi 5,000 kwa viti vya kawaida na 20,000 kwa VIP A na B, tunaomba mjitokeze kwa wingi tusherehekee pamoja,” alisema Kaburu.

Alisema tamasha hilo, litafunguliwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambao ni miongoni mwa wadhamini wao, lakini pia likitarajiwa kupambwa na burudani mbalimbali.

Hadi sasa waliothibitisha ni Bendi ya Twanga Pepeta, wasanii Nassib Abdul ‘Diamond Platinum,’ Dully Sykes, Barnaba Elias na wengine. Mbali na burudani, kutakuwa na utambulisho wa wachezaji wa timu ya vijana na wakubwa, ambapo kabla ya kuanza kwa mechi saa 10.30 jioni, itacheza timu ya vijana Simba dhidi ya Azam FC.

MWISHO wa ngebe ni leo baada ya dakika ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi