loader
Maalim Seif aomba wakulima wa mboga kukopeshwa

Maalim Seif aomba wakulima wa mboga kukopeshwa

Maalim Seif alisema hayo wakati alipotembelea wakulima na wazalishaji wadogo wa mboga kwa kutumia teknolojia ya kisasa huko Dimani mjini hapa.

Alisema taasisi za fedha hazijatoa kipaumbele cha mikopo kwa wakulima wadogo ambao watazalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo chakula na kutosheleza taifa.

“Wakulima wengi hivi sasa wamepiga hatua kubwa na kuweza kuzalisha bidhaa mbalimbali, ikiwemo mboga tatizo ni kwamba hawapati mikopo itakayowasaidia kupata mikopo,” alisema.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili, Affan Othman Maalim alisema baadhi ya miradi ya wazalishaji wa kilimo imeweka malengo zaidi kutoa mikopo kwa akinamama wakulima.

Alisema kama wakulima watapewa nafasi ya kuzalisha mboga nyingi wanaweza kutosheleza soko la sekta ya utalii lililopo nchini.

“Wizara ya Kilimo na Maliasili imeweka mikakati ya kuhakikisha wakulima wetu wanazalisha vyakula, ikiwemo mboga kwa ajili ya kuingia katika soko la kitalii,” alisema.

Aidha alisema Wizara ya Kilimo tayari imeanza utaratibu mzuri wa kutoa dawa kwa wakulima kwa ajili ya kupambana na wadudu wanaoharibu mboga.

Mapema mkulima mmoja wa mboga katika kijiji cha Dunga, Ali Issa alisema ukosefu wa dawa za kupambana na wadudu mbalimbali kwa kiasi kikubwa yamerudisha nyuma maendeleo ya wakulima na kuweza kupiga hatua kubwa ya maendeleo.

UMOJA wa Vijana wa Chama ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi