loader
Dstv Habarileo  Mobile
Madiwani 5 CCM, mmoja CUF wavuliwa udiwani

Madiwani 5 CCM, mmoja CUF wavuliwa udiwani

Akisoma hukumu hiyo kwa zaidi ya saa mbili jana, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Charles Uisso alisema madiwani hao wanavuliwa udiwani huo, kutokana na mahakama hiyo kuridhika na ushahidi wa pande zote mbili, ziliwasilishwa mahakamani hapo wakati wa kipindi chote cha kesi.

Uiso alisema mashitaka dhidi yao, yalipelekwa mahakamani hapo na Mwenyekiti wa Kamati ya Afya, Elimu na Uchumi, Chifu Kalumuna, ambaye ni Diwani wa Kata Kahororo (CCM), akilalamikia madiwani hao ambao walikuwa wajumbe wake katika kamati hiyo, kukaidi kuhudhuria vikao vilivyoitishwa Julai 19, Agosti Mosi, Septemba 23, Novemba 11 na Novemba 14, vyote vya mwaka 2013.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa madiwani hao, walikuwa wakikataa kuhudhuria vikao hivyo muhimu vya kamati hiyo, jambo ambalo lilisababisha kurudisha maendeleo ya wananchi wa Manispaa ya Bukoba.

Hakimu huyo alisema ushahidi wote, uliowasilishwa mahamani hapo kwa pande zote mbili, umeiridhisha mahakama hiyo, kabla ya kutoa hukumu hiyo, kwani mashahidi wote walitoa ushahidi mahakamani hapo.

Madiwani waliovuliwa madaraka na kata zao kwenye mabano ni Samuel Ruangisa (Kitendaguro), Deusdedith Mutakyahwa (Nyanga), Yusuph Ngaiza (Kashai), Dauda Kalumuna (Ijuganyondo), Murungi Kichwabuta (Viti Maalumu), wote wa CCM na mmoja kutoka CUF, Rabia Badru wa Viti Maalumu.

Hata hivyo, mahakama hiyo ilitupilia mbali malalamiko dhidi ya madiwani wengine wawili, Richard Mwemezi wa Kata ya Miembeni (CCM) na Israel Mraki wa Kata ya Kibeta (Chadema), kwa maelezo kuwa hawahusiki moja kwa moja na malalamiko hayo, kwani Richard hakuwa mjumbe wa kamati hiyo na Mraki aliweza kuhudhuria baadhi ya vikao hivyo.

Kwa mantiki hiyo, Mahakama imeelekeza mamlaka husika, Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, kumtaarifu Waziri mwenye dhamana juu ya uamuzi wa mahakama hiyo ili hatua nyingine ziweze kuendelea.

Pia, Mahakama imewaamuru walalamikiwa hao sita waliovuliwa udiwani, kulipa gharama za uendeshaji wa kesi hiyo kwa mlalamikaji aliyepeleka kesi mahakamani.

Hukumu ya kesi hiyo iliyotumia takribani saa mbili, ilivuta hisia za watu mahakamani hapo na kuibua upya makundi ya wanasiasa wenye ushawishi Bukoba, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki na aliyekuwa Meya wa Manispaa hiyo, Dk Anatory Amani aliyevuliwa madaraka kutokana na mambo kutokwenda sawa katika manispaa yake.

Kwa tafsiri ya kesi hii, ni kwamba upande wa wafuasi wa Dk Amani ndiyo wameshinda, kwani mpeleka mashitaka mahakamani ni diwani mshirika wake wa karibu.

Mwaka 2013 Halmashauri ya CCM Mkoa Kagera ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Costansia Buhiye ilitangaza kuwavua udiwani madiwani hao, kwa kosa la kukaidi kuhudhuria vikao hivyo, kabla ya Kamati Kuu ya CCM kuwarejeshea nyadhifa zao.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imepata nmkopo ...

foto
Mwandishi: Angela Sebastian, Bukoba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi