loader
Mafuta kununuliwa kwa M-Pesa

Mafuta kununuliwa kwa M-Pesa

Ushirikiano huo umeanzia kwenye vituo vichache vya Total Tanzania na baadaye unatarajiwa kusambaa maeneo mbalimbali nchini, lengo kuu ni kuhakikisha kila mtanzania anayemiliki chombo cha moto anakuwa na uwezo wa kununua na kulipia mafuta kwa njia iliyo salama na uhakika.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo, Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, alisema siku zote kampuni yake imekuwa mstari wa mbele katika kurahisisha maisha ya Watanzania kupitia miundombinu ya kiteknolojia iliyo nayo.

"Tumekuwa tukibuni njia mbalimbali kila siku kwa lengo la kuwapa urahisi wateja wetu na kuwaondolea adha ambazo wanaweza kuzipata wakiwa wanataka kununua mafuta kutoka vituo vya Total Tanzania, sasa wateja wetu wote kupita M-Pesa ambayo siku izi imechukua nafasi kubwa sana katika mfumo wa maisha ya binadamu wana uwezo wa kununua na kulipia mafuta kutoka vituo hivyo vya mafuta."

Alisema Mwalim Aidha, aliongeza kuwa Vodacom kupitia M-Pesa itaendelea kuwaletea wateja mambo mengi ambayo hayajawahi kutokea nchini, lengo likiwa ni kuhakikisha biashara zote nchini zimeunganishwa na M-Pesa ili kwenda sambamba ambapo hadi sasa tayari biashara zaidi ya 320 zimeshaunganishwa na huduma hiyo.

Meneja wa Maendeleo, Ubora na Mafunzo wa Kituo cha mafuta cha Total Tanzania, Maria Lebby, Amesema kupitia njia hii wateja wa Total watanufaika kutokana na namna kampuni hiyo ilivyo jizatiti katika kurahisisha njia za malipo.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi