Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Minja alitoa mwito huo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Alisema hayo baada ya jeshi hilo kutangazwa kuwa Mshindi wa kwanza kwa upande wa utengenezaji wa bidhaa za samani za ndani katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
“Kuna Maboresho makubwa sana juu ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na Jeshi la Magereza na hiyo ndio imefanya kuibuka mshindi wa kwanza kwa upande wa utengenezaji bora wa samani za ndani,” alisema.