loader
Magufuli: Mshukuruni Kikwete akiwa hai

Magufuli: Mshukuruni Kikwete akiwa hai

Alisema umati uliojitokeza wakati wa ufunguzi wa kituo cha mabasi mjini Mbinga ni sala, na ishara kwamba, Watanzania wanamwombea Rais Kikwete.

“Kwenye watu wengi hawakosi wabaya, wapo wenye wivu, wengine kushukuru kugumu, kushukuru ni mpaka ufe waseme pengo lako halitazibika wakati wameshaliziba,” alisema Magufuli kabla ya Rais kukifungua kituo hicho.

“Wao wengine watakaosema najipendekeza lakini nasema ukweli, na ukweli utabaki kuwa ukweli, na ukweli utabaki ukweli” alisema.

Mbunge wa Mbinga Mashariki, Gaudence Kayombo, alimshukuru Rais kwa niaba ya wananchi jimboni humo na kuongeza kuwa, ni mtu wa watu ndiyo maana anacheza nao.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Saidi Mwambungu alisema katika mkutano huo kwamba ukosefu wa barabara ilikuwa giza kubwa mkoani humo, na kwamba, baadhi ya ndugu walikutana kama msiba kuzungumzia hatma ya wenzao waliokuwa wamepangiwa kwenda.

UJENZI  na ukarabati wa Soko la Kariakoo jijini ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi