loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Makunduchi yaanza vyema Kombe la Majimbo

Mchezo huo wa ufunguzi ulichezwa juzi kwenye Uwanja wa Amaan mjini Unguja na kuhudhuriwa na mashabiki wachache waliofika uwanjani hapo.

Makunduchi ambao walionekana kucheza soka la kupendeza, walipata bao la kuongoza katika dakika ya pili lililofungwa na Mustafa Abdalla huku bao la pili likifungwa dakika ya 44 na Suleiman Ali.

Miamba hiyo iliyokuwa ikishambuliana kwa zamu, ilikwenda mapumziko kwa Jimbo la Makunduchi ikiwa inaongoza kwa mabao 2-1.

Kuanza kwa kipindi cha pili, timu zote ziliingia uwanjani na ari mpya huku kila moja ikiwa tayari imeshapata mawaidha kutoka kwa walimu wao ambapo Makunduchi bila ya ajizi dakika ya 50 waliongeza bao la tatu lililofungwa tena na Abdalla.

Jimbo la Fuoni walijipatia bao la kufutia machozi lililofungwa na Hadid Shaame katika dakika ya sita huku Suleiman Maulid akipaswa kujilaumu baada ya kuikosesha timu yake bao la pili kutokana na kukosa penalti iliyotoka nje katika dakika ya 63.

MWISHO wa ngebe ni leo baada ya dakika ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi