loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mallya yaita watu wakasome michezo

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa chuo hicho, Richard Mganga, kimekuwa kikizalisha wahitimu wenye ujuzi wa kutosha, ambao ikiwa wataajiriwa na kutumiwa vizuri watasaidia kuinua michezo nchini.

“Serikali kwa kupitia Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo ilijenga chuo hiki kwa ajili ya maendeleo ya michezo nchini, hivyo tutumie vizuri fursa hii kuendeleza michezo, katika ngazi mbalimbali,” alisema Mganga.

Mganga alisema sifa za kujiunga na chuo hiko hazitofautiani na vyuo vingine vinavyotoa Stashahada nchini, elimu ya kidato cha nne ambayo itakuwa kwa kiwango cha ufaulu wa “D” tatu au ufaulu zaidi ya hapo, au elimu ya kidato cha sita, na pia uzoefu katika michezo ni muhimu kwa anayetaka kujiunga.

Alisema ikiwa watajiunga watu wengi, itasaidia kupata wataalamu wengi watakaosaidia kuibua vipaji vya michezo sio tu katika klabu maarufu, bali hata kwenye taasisi, halmashauri ambako kuna timu zinazoshiriki mashindano mbalimbali.

Alisema chuo kinatoa Stashahada ya Utawala na Uongozi katika Elimu ya Michezo na Ukocha kwa kuzingatia mitaala ambayo imepitishwa na wataalamu kutoka vyuo vikuu vya kimataifa.

“Chuo kina miundombinu mizuri yakiwemo majengo safi yanayokidhi viwango vinavyohitajika, maktaba nzuri yenye vitabu vya kutosha kwa ajili ya masomo yanayofundishwa, hosteli kwa ajili ya wanachuo yenye uwezo wa kuchukua wanachuo wasiopungua 80,” alisema Mkuu huyo wa Chuo.

Mganga alisema wanajivunia kuwa wanachuo wamekuwa wakijifunza michezo mbalimbali kwa kutumia teknolojia za kisasa. Alisema wanafunzi hujifunza michezo mbalimbali ambayo ni netiboli, mpira wa wavu, riadha, mpira wa mikono, kikapu ambapo pia wana timu za michezo hiyo zinazowawezesha kujifunza kwa vitendo.

MWISHO wa ngebe ni leo baada ya dakika ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi